Marekani yaunga azimio la UN huko Syria

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Samantha power

Mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ameunga mkono- lakini kwa tahadhari uamuzi ulioafikiwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambao unalenga kuhakikisha kuwa msaada wa kibinaadamu unafikishwa nchini Syria.

Mjumbe huyo Samantha Power ameiambia BBC kwamba maneno ya uamuzi huo ni muhimu lakini changomoto kuu itakuwa utekelezaji wake.

Amesema kuwa Urusi ina uhusiano mkubwa na serikali ya rais Bashar al-Assad na hivyobasi inafaa kuhakikisha kuwa serikali ya Syria inazingatia uamuzi huo.

Miongoni mwa hatua za azimio hilo ni mahitaji ya kufungua mpaka wake ili kuruhusu misaada kuingia nchni humo,kusitisha urushaji wa mabomu mbali na kutotumia njaa kama silaha ya vita.

hatahivyo waandishi wetu wanasema kuwa azimio hilo huenda ni hafifu kwa kuwa halitoi vikwazo vyovyote dhidi ya serikali ya Syria iwapo itakataa kuzingatia mahitaji hayo.