Kamanda mkuu wa Taliban auawa Pakistan

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wapatanishi katika mazungumzo kati ya serikali ya Pakistan na Taliban

Kamanda mkuu wa Taliban nchini Pakistan, Asmatullah Shaheen ameuawa kwa kupigwa risasi katika ngome ya kundi hilo Kaskazini ya Waziristan.

Eeneo hilo liko karibu na mpaka na Afghanistan.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Maafisa wa usalama na jamaa za kamanda huyo.

Asmatullah Shaheen alivamiwa alipokuwa anasafiri kupitia katika kijiji kilichoko karibu na eneo la Miranshah Kaskazini mwa Waziristan.

Maafisa wengine wawili wa kundi hilo pia waliuawa.

Haijulikani nani aliyewaua Miransah na maafisa wake wawili wala hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa wapiganaji hao.

Shaheen alikuwa naibu mkuu wa kundi hilo baada ya kamanda mkuu wa Taliban nchini Pakistan Hakimullah Mehsud kuuawa mwaka jana.