"Wanataka kuniua", Adai Biti

TendaI Biti
Image caption Waziri wa zamani Zimbabwe ambaye pia ni mwanachama mashuhuri wa upinzani

Waziri wa zamani wa Fedha nchini Zimbabwe ambaye pia ni mwanasiasa mashuhuri wa Upinzani, Tendai Biti amelalamikia jaribio la kumuua baada ya bomu kurushwa ndani ya makaazi yake.

Hakuna majeruhi wowote kwenye tukio hilo la Jumanne. Mwandishi wa BBC nchini Zimbabwe amesema hajabainishwa aliyehusika na shambulio hilo.

Katika siku za karibuni kumeripotiwa malumbano makali ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement For Democratic Change-MDC. Afisa mmoja wa upinzani amedai kwamba shambulio hilo limetekelezwa na chama tawala cha ZANU-PF.