Zenit yalazwa 4-2 na Borussia

Image caption Lewandowski

Klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund iliyomaliza ya pili msimu uliopita ilijihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika ligi kuu ya mabingwa Barani ulaya ilipoibana Zenit St Petersburg nyumbani kwao mabao 4-2.

Wafungaji wa Dortmund walikuwa ni Henrikh Mkhitaryan kunako dakika ya tano.

Marco Reus, alifunga dakika mbili baadaye naye Robert Lewandowski akafunga mawili kunako dakika 61′, 71′ .

Mabao ya Zenit yakifungwa na Oleg Shatov57′ na Hulk 69′ .

Mechi zingine mbili zimeratibiwa kuchezwa leo kubwa ikimjumuisha aliyekuwa mshambulizi machachari wa Chelsea Didier Drogba ambaye anakabiliana na kocha wake wa zamani Jose Mourinho wa Chelsea timu yake ya Galatasaray ya Uturuki ikiialika Chelsea mjini Instabul.

Mourinho ambaye amejipata matatani kamera zilipomnasa akimkejeli mshambulizi wake matata Samuel etoo Kutoka Cameroun kuhusiana na umri wake anatazamiwa kuiongoza Chelsea kuvunja msururu wa bahati mbaya kwa timu za uingereza katika mshindano ya msimu huu .

Katika ile mechi nyingine Vinara wa ligi kuu ya Uhispania La liga real Madrid ambao wameipiku Barcelona kileleni mwa jedwali la La liga watakuwa Ujerumani kwa mwaliko wa Shalke 04 ya Ujerumani .