Ufaransa yazuia washukiwa kurudi Rwanda

Haki miliki ya picha none
Image caption Watutsi wengi waliuawa wakati wa mauaji ya Kimbari mwaka 1994

Mahakama nchini Ufaransa, imezuia mipango ya kuwarejesha nyumbani washukiwa watatu wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994, kuhukumiwa mjini Kigali.

Mahakama hiyo iliamua kuwa wanaume hao hawataweza kufunguliwa mashitaka nchini Rwanda, kwa kosa ambalo halikufafanuliwa kisheria wakati ambapo uhalifu huo ilitokea.

Mauaji ya kimbari yalianza kuwa kosa la kuadhibiwa nchini Rwanda chini ya sheria ambazo zilipitishwa kati ya mwaka 1996 hadi 2004.

Takriban watu 800,000 wengi wa kabila la Tutsi na wachache wa Hutu, waliuawa kwenye vita vya kikabila mwaka 1994.

Wapiganaji kutoka kabila la Hutu walituhumiwa kwa kufanya mauaji hayo.

Mahakama ilibatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama ya Rufaa mwaka jana na kuidhinisha kuhamishwa kwa Claude Muhayimana na Innocent Musabyimana kukabiliana na kesi dhidi yao nchini Rwanda.

Pia ilisisitiza kusalia kwa hukumu ya mahakama iliyotolewa mwezi Septemba , ikakatalia mbali kuhamishwa kwa Laurent Serubuga nchini Rwamba.

Alikuwa naibu mkuu wa jeshi wa Rwanda wakati mauaji ya kimbari yalipofanyika.

Bwana Muhayimana, ni raia wa Rwanda na Ufaransa na anatuhumiwa kwa kushiriki mauaji ya Watutsi mjini Kibuye magharibi mwa Rwanda.

Naye Bwana Musabyimana anadaiwa kuhusika na mauaji katika mkoa wa Gisenyi.

Mwezi Julai mwaka jana Bwana Serubuga alizuiliwa nchini Ufaransa baada ya kutolewa kibali cha kumkamata na mahakama ya Rwanda.