Jeshi la Urusi laruhusiwa kwenda Crimea

Bunge la Crimea linapepea bendera ya Urusi Haki miliki ya picha Reuters

Bunge la Urusi limeidhinisha ombi la Rais Putin kuwa wanajeshi wa Urusi watumike Ukraine.

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Urusi imesema hiyo haimaanishi kuwa wataanza kutumika moja kwa moja, ingawa wakuu wa Ukraine wanasema Urusi imeshatuma wanajeshi 6,000 zaidi huko Crimea.

Kikosi cha wanamaji wa Urusi katika Black Sea kimesema kuwa wanajeshi wake wanapiga doria pamoja na wenyeji wa Crimea wanaounga mkono Urusi, ili kulinda vituo vyake.

Mwandishi wa BBC alioko Sevastopol anasema wanajeshi wanaonekana zaidi.

Meli za Ukraine za kulinda pwani zimeondoka kuepuka kuchukuliwa na Urusi na mwandishi wa BBC anasema kuna hisia kuwa ras wa Crimea inazidi kuwaponyoka wakuu mjini Kiev.