Kesi ya Oscar Pistorius yaanza A. Kusini

Haki miliki ya picha e
Image caption Oscar Pistorius

Kesi dhidi ya bingwa wa mashindano ya Olimpiki kwa wanariadha walemavu kutoka Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeanza kusikilizwa

Anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi Februari mwaka jana.

Mahakama mjini Pretoria ilimuachilia Pistorius kwa dhamana ya randi millioni moja, sawa na kiasi ya Dola laki moja.

Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentines mwaka jana.

Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.