Mawakili wa Pistorious wahoji shahidi

Oscar Pistorious Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwanariadha mlemavu Oscar Pistorious akiwa mahakamani

Mawakili wa mwanariadha maarufu wa Afrika kusini Oscar Pistorius wameanza tena kumhoji shahidi muhimu .

Kesi ya Bwana Pistorius ilianza hapo jana (Jumatatu) katika makama mjini Pretoria.

Jana shahidi mmoja wa upande wa waendesha mashitaka, Michelle Burger ambaye ni jirani wa Bwana Pistorius aliieleza mahakama kuwa alisikia kile alichokitaja kama kelele za mauaji zikitoka katika nyumba anamoishi Pistorious, zilizofuatiwa na milio ya bunduki, katika usiku ule alipomuua mpenzi wake.

Mwanariadha huyo wa Olympic ambaye miguu yake imekatwa na ambaye hukimbia kwa kusaidiwa na miguu bandia anasema, alimpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia baada ya kudhania kuwa alikuwa ni mtu mwingine alievamia nyumba yake.