Putin ashutumu mapinduzi nchini Ukraine

Haki miliki ya picha
Image caption Rais Vladimir Putin wa Urusi

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema matukio yaliyomng'oa madarakani rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych yanatokana na "ukiukaji wa katiba na uporaji wa madaraka kijeshi."

Amesema"wanamgambo" wameitumbukiza nchi hiyo katika "vurugu".

Bwana Putin amesema Bwana Yanukovych alikubali mambo yote yaliyotakiwa na upinzani.

Vikosi vya Urusi na Ukraine katika jimbo la Crimea nchini Ukraine viko katika hali ya tahadhari, lakini wasiwasi uliokuwa umetanda kuwa Urusi ingefanya shambulio la kijeshi nchini Ukraine, kwa sasa umepungua.