Wanajeshi watano wauawa Afghanistan

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vikosi vya Marekani vimekua vikiongoza vikosi vya kimataifa kupambana na wanamgambo wa kiislam

Wanajeshi watano wa Afghanistan wameuawa na wengine wamejeruhiwa katika jimbo la Logar.Maafisa wa Afghanistan wamesema kuwa walilengwa kimakosa na Ndege isiyo na rubani ya Marekani.

Majeshi ya jumuia ya kujihami, NATO yametoa salamu za rambirambi kwa familia za wanajeshi na kuanzisha uchunguzi ili kubaini namna tukio hilo lilivyotokea.

Rais wa Afganistan, Hamid Karzai,amekua akikosoa Operesheni na mashambulizi ya anga yanayofanywa na Vikosi vya kimataifa ambavyo vimegharimu maisha ya Raia wa nchi hiyo.

Karzai alikataa kutia saini makubaliano na marekani ya kuridhia kubaki kwa sehemu ya vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan, baada ya kumalizika kwa Operesheni yao mwaka huu.