Kombe la dunia labisha hodi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikosi cha England

Hapo jana kulichezwa mechi kadhaa za maandalizi ya kushiriki katika kombe la dunia litakalochezwa miezi mitatu ijayo huko Brazil.

Na Brazil ilionyesha makali yake katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bafanabafana ya Afrika Kusini kwa kuichapa mabao matano kwa bila nchini Afrika kusini.

Mchezaji matata Neymar alikuwa miongoni mwa wale waliovuruga lango la Afrika Kusini kwa makombora na kuicha Afrika kusini taaban baada ya kuandaa kombe hilo mwaka wa 2010.

Na Ghana inayowakilisha bara la Afrika katika kindumbwendumbwe ilianza kampeni yake vibaya kwa kuchapwa bao moja kwa sufuri Montenegro.

Dejan Damjanovic ndiye aliyefunga bao hilo la pekee.

Katika Mechi nyingine Engalnd iliizaba Denmark bao moja kwa bila lililofungwa na Daniel Sturidge

Kwengineko Colombia ilitoka sare na Tunisia ya bao moja kwa moja japo udhaifu wa Colombi ulionekana kwa kukosekana kwa mchezaji nyota Radamel.

Colombia, imo katika kundi moja na ndovu wa Afrika ya magharibi Ivory Coast na Japan.