Walioteka bandari Libya wauza mafuta nje

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kundi la wapiganaji wa Libya

Wanamgambo walioteka bandari ya nchini Libya wameiambia BBC kuwa wameanza kusafirisha mafuta kwenda nchi za nje kwa meli ya kwanza iliyopeperusha bendera ya Korea ya Kaskazini.

Naibu wa Waziri wa Mafuta ameithibitishia BBC kuwa meli hiyo ya mafuta Morning Glory ilitia nanga katika bandari ya Sidr iliyochini ya himaya ya wanamgambo.

Uwezo wa serikali ya Libya kuhuisha biashara ya kusafirisha mafuta nje ya nchi ambayo ni muhimu kwa kuimarisha uchumi wa nchi hiyo zilikumbana na vikwazo vya migomo na maandamano na bandari na visima vya mafuta kutekwa na wanamgambo maeneo mbali mbali nchini humo.