Ndege ya Malaysia yapotea na abiria 239

Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi ya ndugu wa abiria waliopotea na ndege ya shirika la ndege la Malaysia wakilia kwa uchungu

Juhudi za kimataifa zinaendelea kutafuta ndege ya shirika la ndege la Malaysia iyokuwa ikielekea Beijing nchini China na kupotea baharini ikiwa na abiria 239.

Ndege hiyo iliyopotea aina Boeing 777 ilkuwa na abiria wapatao 239 pamoja na wafanyakazi wa ndege

Asia ya Kusini Mashariki imeongeza nguvu katika juhudi hizo za kutafuta ndege hiyo iliyopotelea katika eno la bahari la Malaysia na Vietnam .

Shirika la ndege la Malaysia limesema ndege hiyo namba MN370 ilipotea majira ya saa 8:40 kwa saa Malaysia siku ya Ijumaa baada ya kuondoa Kuala Lumpur.

Jeshi la Malaysia limesema kikosi cha pili cha helikopta na Meli kimetumwa kwenye eneo la tukio lakini hata hivyo hakuna chochote kilichoonekana katika hatua za awali za utafutaji wa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili Beijing China majira ya saa 12:30 kwa saa za Malaysia.

Waziri wa Usafiri wa Malaysia amesema hakuna taarifa za zozote za kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo.

"Tunafanya kila linalowezekana ndani ya uwezo wetu kujua ndege hiyo ilipo," Hishammuddin Hussein amewaambia waandishi wa habari katika mji Kuala Lumpur