Watawa waachiliwa huru Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watawa walioachiliwa huru nchini Syria

Imethibitishwa kuwa waasi nchini Syria, wamewaachilia huru watawa kumi na watatu na wafanyikazi watatu wa nyumbani waliotekwa nyara mwaka jana.

Watawa hao waliwasili katika mjini deidet Yabus karibu na mpaka wa Lebanon baada ya safari ya saa tisa.

Mwandishi wa habari wa shirika la habari la Ufaransa, amesema kuwa watawa hao walionekana kulemewa na uchovu, na wawili kati yao walibebwa kutoka kwa magari yao.

Watawa hao walitekwa nyara kutoka kwa hekalu moja kati mji wa kale wa Maaloula Desemba mwaka uliopita, baada ya kutekwa wa waasi wa Kiislamu.

Generali mmoja wa Lebanon ambaye aliongoza mazungumzo ya kuachiliwa kwao, amesema serikali ya Syria itawaachilia huru zaidi ya wafungwa mia moja na hamsini wa kike wanaozuliwa.