Colorado yanufaika na uuzaji wa Bangi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bangi inayouzwa Colorado

Utawala wa jimbo Colorado nchini Marekani,umesema kuwa katika kipindi cha siku za kwanza thelathini tangu ukuzaji na uuzaji wa bangi kuhalalisha, umekusanya zaidi ya dola milioni mbili kama ushuru.

Jimbo hilo ndilo eneo la kwanza duniani kuwahi kuhalalisha uuzaji wa bangi kwa matumizi wa starehe.

Kwa mujibu wa takwimu bangi inayokisiwa kugharimu dola milioni kumi na nne iliuzwa mwezi Januari, wakati sheria hiyo ilipoanza kutekelezwa.

Utawala wa jimbo hilo umesema kuwa ushuru huo utatumiwa kujenga shule.

Ruhusa uuzaji wa bangi na ushuru utaongezeka maradufu, ni moja kati ya masuala yaliyopogiwa debe na wanaharakati wanaunga mkono matumizi ya bangi katika jimbo Colorado.

Haki miliki ya picha non BBC
Image caption Watu wakivuta bangi Colorado

Na ikiwa takwimu za uuzaji huo katika mwezi wa kwanza ni za kuaminika, basi utawala wa jimbo hilo unajiandaa kupokea fedha zaidi za matumizi kutoka na ulevi huo wenye utata.

Bangi yenye dhamani ya dola milioni kumi na nne iliuzwa Januari pekee, wakati sheria hiyo ilioidhinishwa.

Jimbo lanufaika na Bangi

Wapiga kura waliidhinisha sheria hiyo baada ya kura ya maoni katika majimbo ya Colorado na Washington licha ya kuwa serikali ya Marekani, ingali imeorodhesha bangi kama dawa ya kulevya.

Jimbo la Colorado, ilikuwa jimbo la kwanza kuruhusu maduka kuuza bangi na inatoza ushuru wa uugizaji na uuzaji.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bangi inayouzwa Colorado

Kuambatana na sheria hiyo dola milioni arubaini ya kwanza itakayokusanywa kama ushuru itatumiwa kujenga shule zaidi.

Hata hivyo bado kuna mjadala mkali si tu kuhusu swala hilo nyeti la kuruhusu uzwaji bangi, lakini pia khusu ni mradi upi utafadhiliwa baada ya mradi huo wa ujenzi wa shule kukamilika .

Baadhi ya raia nao wanataka fedha hizo kutumiwa kuthibiti uuzaji na ukuzaji wa bangi nao wengine wakipendekeza kutumiwa kwa kampeini ya kuwahimiza watoto kutojiingiza katika tabia ya uvutaji bangi na pia kupigia debe kampeni ya kuwashawishi watu wasiendeshe gari wakiwa wamevuta bangi.