Maandamano Juba kupinga UN

Imebadilishwa: 11 Machi, 2014 - Saa 07:34 GMT

Maandamano Sudan Kusini

Zaidi ya watu 1,000 waliandamana Jumatatu mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini , huku wakituhumu Umoja wa Mataifa kwa kuwahami waasi.

Mnamo siku ya Ijumaa,serikali ilisema kuwa wanajeshi wake walinasa silaha kwenye msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa ambao yaliyokuwa yameandikwa chakua cha msaada.

Umoja wa Mataifa umekanusha madai hayo ya kuwapa waasi silaha lakini ukasema kuwa ulikosea kusafirisha silaha hizo kwa barabara.

Umoja huo una walinda amani 8,000 Sudan Kusini, taifa changa zaidi duniani ambako mgogoro wa kisiasa ulizuka Disemba kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Mwezi Januari, Rais Salva Kiir alituhumu Umoja wa Mataifa kwa kuendesha Serikali mbadala nchini mwake, madai ambayo UN ilikanusha.

Duru zinasema kuwa tukio la hivi karibuni, huenda likakithirisha uhasama wa serikali dhidi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.

Waandamanaji hao walimtaka mjumbe maalum wa UN nchini Sudan Kusini Hilda Johnson kujiuzulu.

Waandamanaji hao walihutubiwa na maafisa wakuu wa serikali.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa ,Ariane Quentier aliambia BBC kuwa wajumbe wa Umoja wa Mataifa watawasili nchini humo Jumanne kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na serikali ya Sudan Kusini kuhusu madai hayo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.