Vigogo wa kisiasa mahakamani Sudan:K

Image caption Pagan Amum (Kulia)

Kesi imeanza nchini Sudan Kusini ya vigogo wanne wa kisiasa wanaotuhumiwa kwa uhaini kwa madai ya kujaribu kumwondoa mamlakani Rais Salva Kiir baada ya vita kuzuka mwaka jana.

Washitakiwa ni pamoja na Pagan Amum, aliyekuwa katibu mkuu wa chama tawala , mawaziri wa zamani na walinzi pamoja na balozi wa zamani nchini Marekani.

Wote wamekanusha madai hayo.

Maelfu ya watu wameuawa katika vita kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wanaomuunga mkono Riek Machar.

Makabiliano yameendelea licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa mwezi Januari.