Marekani yasusia mazungumzo na Urusi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani haiiungi mkono Urusi kuvamia mji wa Crimea

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amekataa kukutana na Rais wa Urusi, Vladmir Putin, mpaka pale Moscow itakaporidhia mapendekezo ya Marekani kuhusu kumaliza mzozo nchini Ukraine.

Kerry amemwambia waziri wa mambo ya nje wa Urusi kuwa uvamizi wa kijeshi wa Urusi mjini Crimea umefanya mazungumzo ya kufikia muafaka kuwa magumu mno.

Maafisa wa Marekani wamesema ikiwa kura ya maoni iliyopendekezwa itapigwa mwishoni mwa juma kuhusu kuridhia kwa Crimea kuwa sehemu ya Urusi, hakuta kuwa na suala jingine la kuzungumza.

Maafisa hao wamesema kuwa ikiwa hali itafikia hivyo, Marekani itaiwekea Urusi vikwazo vikali.