Kampuni ya mafuta kuchunguzwa-Goodluck

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Goodluck Jonathan

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan, ameagiza kufanyika kwa uhasibu wa kina kufanyika katika kampuni ya taifa ya mafuta, kufuatia madai kuwa zaidi ya dola bilioni ishirini ya mapato ya kampuni hiyo imetoweka.

Mwezi uliopita, gavana wa banki kuu ya Nigeria, Lamido Sanusi, alisimamishwa kazi baada ya kusema kuwa Shirika la kitaifa na mafuta nchini humo, NNPC, lilikuwa limeshindwa kuelezea kuhusu fedha hizo.

Waziri wa fedha Ngozi Okonji-Iwela na kamati ya fedha ya bunge la Seneti ambao wanachunguza madai hayo, wametoa wito wa kufika kwa uhasibu wa vitabu vyote vya hesabu ya shirika hilo la NNPC tangu wakati huo.