IGAD kupatanisha mahasimu Sudan.K

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgogoro wa Sudan Kusini ungali unatokota

Viongozi wa muungano wa kuichumi na maendeleo kanda ya Afrika Mashariki na kati IGAD, leo wanakutana kwa kikao maalum mjini Adis Ababa nchini Ethiopia kujadili mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Sudan Kusini.

Mkutano huo unaofanyika Addis Ababa, unajiri baada wa makamishna walioteulia na Muungano wa Afrika kuchunguza ghasia na machafuko ya Sudan Kusini kuanza kazi yao siku ya Jumatano baada ya kuapishwa.

Lengo la mkutano huo,ni kujaribu kutekeleza mkataba wa kusitisha vita kati ya pande zinazozana uliotiwa saini mwezi Januari ingawa umekosa kusitisha vita hivyo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir -- ambaye vikosi vyake vinapambana na waasi wanaomtii aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar -- anatarajiwa kuhudhuria kikao hicho.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu milioni moja wametoroka majumbani kwao huku maelfu wengine wakifariki tangu kuzuka vita hivyo mwezi Disemba mwaka jana.