Wanajeshi sita wauawa Misri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanajeshi akishika doria Misri

Watu wasiojulikana wamewashambulia wanajeshi waliokuwa wanashika doria katika kizuizi cha barabarani viungani mwa mji mkuu Misri.

Wanajeshi sita waliuawa.

Mabomu mawili yaliteguliwa karibu na kizuizi hicho.

Shambulizi hilo lilifanyika wakati wanajeshi walipokuwa wanasali na lilikuwa shambulizi la pili kufanyika katika kipindi cha siku tatu.

Mnamo siku ya Alhamisi, watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao walishambulia basi la wanajeshi mjini Cairo na kumuua mwanajeshi mmoja wengine watatu wakijeruhiwa.

Jeshi limelaumu kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kwa kufanya mashambulizi hayo ingawa limekuwa likikanusha.