Jeshi la Syria lakomboa mji muhimu

Mji wa Yabroud ukishambuliwa Haki miliki ya picha AP

Serikali ya Syria imeukomboa mji wa Yabroud, ngome ya wapiganaji, karibu na mpaka wa Libnan.

Televisheni ya Hezbollah, Al Manar, imekuwa ikionyesha wanajeshi wa Syria katikati ya mji huo ambao unaonekana umehamwa.

Wapiganaji Waislamu wanaopinga serikali wanasema walitoka mjini humo baada ya kuzingirwa.

Mji wa Yabroud umekuwa ukishambuliwa kwa mabomu kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Piya ulikuwa muhimu kwa wapiganaji kwa sababu ndiko bidhaa muhimu zinaweza kupitishwa kutoka Libnan, na piya ni njia inayounganisha miji ya Damascus na Aleppo kuelekea mwambao wa Syria.