Dini kupambana na utumwa mamboleo

Haki miliki ya picha unknown
Image caption Utumwa mamboleo

Mpango wa pamoja kukabiliana na utumwa mamboleo pamoja na biashara haramu ya binadamu umezinduliwa na Kanisa Katoliki, Kanisa la kianglikana na Uongozi wa Waislam wa Ki-sunni ambao kiongozi wake ni Imamu wa chuo kikuu cha al Azhar.

Mpango huo wa Global Freedom Network umezinduliwa Vatican na unanuia kupambana na utumwa kwa kuhimiza serikali, makundi ya wafanyibiashara, waumini na wasomi kumaliza mitandao ya utumwa.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu millioni thelathini wamezuiliwa kote duniani na kulazimishwa kuwa wafanyikazi wa nyumbani, watumwa wa ngono, watoto wanaotumiwa kama wanajeshi na wafanya kazi nyingine za mikono.

Mpango huu utashirikiana na kikundi cha wanaharakati cha Free Foundation.