Wanajeshi 5 wauawa Benghazi, Libya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanajeshi wa Libya

Wanajeshi watano wameuawa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari.

Bomu hilo lililipuka nje ya kambi ya jeshi mjini Benghazi Mashariki mwa Libya.

Zaidi ya wengine kumi wamejeruhiwa vibaya.

Bomu hilo lililipuka wakati watu waliokuwa wamehudhuria sherehe za mahafali wa jeshi wakiondoka katika sherehe hizo.

Hili ni shambulizi la hivi karibuni kukumba maeneo yanayozingira mji wa Benghazi, ambao ulikuwa kitovu cha maandamano yaliyomwondoa mamlakani hayati Muammar Gaddafi.