Mpenzi wa Mick Jagger ajitoa uhai

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mick Jagger ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha mpenzi wake L'Wren Scott

Mwanamitindo wa kimataifa na mpenzi wa mwanamuziki, Mick Jagger, L'Wren Scott, amepatikana akiwa amefariki nyumbani kwake mjini New York, Marekani.

Scott, mwenye umri wa miaka 49, alipatikana na msaidizi wake nyumbani kwake saa nne za asubuhi saa za New York.

Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alijitoa uhai, ingawa madaktari wanachunguza kilichomuua.

Msemaji wa Sir Mick, ameelezea kuwa Mick ameshtushwa sana na kifo cha mpenzi wake.

Micka humba katika bendi ya Rolling stone na kwa sasa bendi hiyo iko katika ziara ya kutumbuiza mashabiki nchini Australia.

Scott alianza kazi yake ya uanamitindo mjini Paris kisha akahamia mjini Los Angeles na kuanza kazi ya kuunda mitindo mbali mbali,

Marehemu Scott na Muimbaji Mick walianza uhusiano wao mwaka 2001.

Kifo cha Scott kimetokea mwezi mmoja baada ya kufutilia mbali maonyesho ya mitindo yake mjini London.

Huku taarifa za kifo chake zikiendlea kuenea, tayari rambi rambi zimeanza kumiminika kutoka kote duniani.