Tuzo ya mwalimu bora duniani yazinduliwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bill Clinton ndiye mwenyekiti wa wakfu huo

Tuzo ya mwalimu bora zaidi duniani imezinduliwa.

Tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni moja, itakabidhiwa mwalimu ambaye anafanya kazi ya ualimu na ambaye atathibitisha kuwa mchango wake kwa jamii umekuwa bora zaidi kuliko walimu wengine wote duniani.

Pesa hizo zitatolewa kwa kipindi cha miaka kumi, lakini mwalimu huyo ataendelea kufundisha angalau kwa miaka mingine 5.

Tuzo hiyo ambayo imezinduliwa na wakfu wa Varkey Gems, shirika ambalo hutoa mchango mkubwa katika sekta ya elimu duniani, inaungwa mkono na mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum.

Mwenyekiti wa wakfu huo ni Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Bwana Clinton amesema kuwa ni muhimu sana kuwavutia watu bora zaidi kuwa walimu na pia kuwaza kuwathamini na kuthamini kazi zaO.

Unadhani mwalimu wako anaweza kushinda tuzo hii?