Njama ya mashambulizi yatibuliwa Kenya

Image caption Mji wa Mombasa umekuwa ukishuhudia machafuko yanayosababishwa na vijana wanaokumbatia itikadi kali za dini

Polisi mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewakamata watu wawili waliokuwa na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari lao

Kwa mujibu wa polisi washukiwa hao mmoja raia wa Kenya na mwingine msomali, walikuwa wanajiandaa kufanya mashambulizi katika eneo lisilojulikana.

Inaarifiwa polisi waliwakamata baada ya kupata taarifa kuhusu njama yao.

Vyombo vya habari vinasema kuwa usalama umedhibitiwa mjini humo kufuatia tukio hilo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii