Hospitali ya watoto ya N.Mandela yaanza kujengwa

Image caption Afrika Kusini inakabiliwa na uhaba wa hospitali za watoto

Ujenzi wa Hospitali ya watoto iliopewa jina la Nelson Mandela Children Hospital umeanza mjini Johannesburg.

Hospitali hio itakua na vitanda Zaidi ya 200 ikiwa na uwezo wa kutibu magonjwa mbali mbali ya watoto nchini A-Kusini na pia barani Afrika .

Kumekuwepo uhaba wa Hospitali za watoto barani Afrika na hii itakua Hospitali ya 5 inayotarajiwa kuwa kubwa kuliko zote .

Ujenzi wa Hospitali hii ya watoto iliopewa jina la Nelson Mandela ulizinduliwa na waziri wa Afya wa Afrika Kusini Aroun Mosoeledi chini ya udhamini wa wakfu wa Nelson Mandela.

Bi Bongi Mkabela afisa mkuu wa wakfu wa Hospitali hii ya watoto anasema wamehakikisha wanazo nusu ya pesa wanazohitaji, dola million 50 ndipo wameamua ujenzi huu.

Ameongeza kuwa wakfu wa Bill and Melinda gates wa Marekani pia umetoa mchango wake.

Prof Keith Bolton ambae ni mshauri wa magonjwa ya watoto amesema tangu Afrika Kusini ijikomboe kutoka utawala wa ubaguzi wa rangi miaka 20 iliopita, ni Hospitali Moja tu ya watoto iliyo mjini Capetown iliojengwa miaka 50 iliopita na hili limekua tatizo kubwa sana kwa watoto kupata matibabu A-Kusini.

Mjini Johannesburg peke yake utakuta kuna watoto zaidi ya 350 wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo na wengi hufariki kabla ya zamu yao kufikia.

Bi Bongi mwenyewe alimpoteza mwanawe katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya mwanawe kulazwa kwa muda wa mwezi mmoja.

Hii ndio moja ya sababu iliomfanya Marehem Nelson Mandela kuamua pawepo Hospitali rasmi ya watoto.

Na Marhemu Nelson Mandela aliusia kabla ya kufa kwake kuwa Hospitali hio ikijengwa lazima iwahudumie na watoto walioko katika mataifa ya Kusini mwa Afrika