Wakeketaji mahakamani Uingereza

Haki miliki ya picha v
Image caption Licha ya kuharamishwa, ukeketaji unafnya sana uingereza miongoni mwa jamii ya wasomali na waarabu

Maafisa nchini Uingereza wamesema kuwa wamewachukulia hatua za kisheria madaktari waliomkeketa mwanamke mmoja nchini humo.

Daktari , Dhanoun Dharmasena, anadaiwa kumfanyia kitendo hicho mwanamke mmoja punde baada ya kujifungua katika hospitali moja mjini London.

Mshukiwa wa pili, Hassan Mohamed, anatuhumiwa kumsaidia daktari Dhanoun katika kutekeleza kitendo hicho.

Wawili hao ni washukiwa wa kwanza kuwahi kufikishwa mahakamani kwa kufanya kitendo hicho ambacho kimeharamishwa nchini humo.

Sheria hiyo imekuwepo tangu mwaka 1985.

Duru zinasema kuwa Uingereza haijakuwa na rekodi nzuri ya kuwashitaki wakeketaji kama vile Ufaransa ambapo zaidi ya watu 100 wameshitakiwa kwa kuwakeketa wanawake.