Mradi wa umeme DRC kudhaminiwa

Bwawa la Inga Haki miliki ya picha
Image caption Mradi wa umeme katika bwawa la Inga DRC

Benki ya dunia imeidhinisha msaada wa kitita cha dola milioni sabini na saba kuisaidia Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo kuendeleaza mradi wa bwawa la umeme.

Benki ya dunia imesema pesa hizo , pamoja na dola milioni thelathini na tatu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika zitadhamini uchunguzi wa kina wa athari za kimazingira katika bwawa umeme la Inga na kuhakikisha mradi huo unaimarika .

Makampuni matatu ya kimataifa yamepata kandarasi ya kujenga mabwawa mengine kutoka kwa bwawa hilo yajulikanayo kama Inga Three.

Waziri mkuu wa Kongo Augustin Matata Ponyo amesema mradi huo ni wa mafanikio makubwa kwa Afrika katika karne ya 21 .

Waandishi wa habari wanasema mabwawa mawili yaliyopo kwa sasa yalijengwa miongo kadhaa na yameharibika baada ya kutelekezwa na ukosefu wa uwekezaji katika miundo mbinu hiyo muhimu.