Mabaki ya ndege ya Malaysia yatafutwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Shughuli ya Kutafuta mabaki ya ndege ya Malaysia zanza tena.

Ndege na meli kutoka mataifa mbalimbali yameanzisha upya kutafuta mbaki ya ndege ya shirika la Malaysia

iliyotoweka hewani zaidi ya majuma mawili yaliyopita ikiwa na karibu abiria 240.

Matumaini ya kusuluhisha jinamizi hiyo yalipanda wakati Australia ilipotoa picha zilizochukuliwa na mtambo wa satellite

zikionyesha vitu viwili katika Bahari, laki Alhamisi hakuna kitu kilichopatikana wakati ndege zilipopaa katika eneo hilo

kutafuta.

Afisa wa cheo cha juu kutoka New Zealand alisema shughuli hizo za kutafuta ndege hiyo zilivurugwa na Bahari

iliyochafuka na ilikuwa vigumu kuona cho chote.

Ndege ya mizigo Norway ilitumia mataa makubwa ya usiku kutafuta mabaki ya ndege katika eneo hilo lakini hakuna kilichopatikana.