Thamani ya Tausi waijua polisi Pakistan

Tausi Haki miliki ya picha R DAKIN
Image caption Tausi wa Pakistan

Polisi watatu wanaolinda makazi ya waziri mkuu wa Pakistan wamesimamishwa kazi kwa muda baada ya Paka kumuua Tausi wa waziri mkuu.

Mtunza bustani alipata Tausi mmoja amekufa katika moja ya bustani za makazi ambapo ndege hao huvinjari , lilieleza gazeti la Express Tribune.

Mmoja wa maafisa waliosimamishwa kazi amesema wengine 21 waliitwa kujieleza baadae. Imeripotiwa kuwa maafisa hao walisema walikuwa kazini usiku ule , lakini hawakutegemea kuwa Paka wangemla Tausi.

Maafisa 18 hawakubainika kuwa na hatia, gazeti lilieleza.

Lakini watatu waliosalia wote walipewa onyo na kuadhibiwa kwa uzembe

Makazi ya waziri mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif yako Raiwind, viungani mwa mji wa Lahore.