Picha ya 'mabaki ya ndege' iliyopotea

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Picha za Satelite ambazo China inasema huenda ni mabaki ya ndege iliyopotea

China imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege kwenye eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.

Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa wa Malaysia wanasema.

Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.

Amesema serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.

Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea kwenye masiliano ilipokuwa imeondoka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 ikiwa na abiria 239.