Crimea kuugubika mkutano wa G7

Mzozo kuhusu Crimea na Ukraine utajadiliwa leo na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo rais Obama.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Obama akitoa taarifa rasmi baada ya unyakuzi wa Crimea

Viongozi hao wamejumuika katika kongamano la kujadili usalama wa nyuklia lakini ajenda hio inatarajiwa kugubikwa na mazungumzo kuhusu hatua ya Urusi kunyakua eneo la Crimea.

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesusia mkutano huo na kumtuma waziri wake wa maswala ya kigeni.

Rais Obama,Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na viongozi wenzao kutoka mataifa saba yaliyoendelea zaidi watakutana katika kikao maalum kuzungumzia hatua zaidi za kuiadhibu Urusi.

Huenda Moscow ikatengwa zaidi katika maswala ya kisiasa na kiuchumi.Tayari mataifa ya Ulaya yameapa kuiwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii