Alshabaab wautoroka mji wa Koryoley

Haki miliki ya picha AFP

Vikosi vya umoja wa Afrika pamoja na wanajeshi wa Somali wamepiga kambi kandokando ya mji wa Koryoley ambao wameuteka kutoka kwa kundi la Alshabaab baada ya makabiliano makali.

Mamia ya wanajeshi wa Uganda waliwalazimishi wapiganaji wa alshabaab kuukimbia mji huo ikiwa ni mara ya kwanza kwa mji ulio kusini mwa somali kuchukuliwa na vikosi hivyo.

Baadhi ya raia pamoja na wanajeshi waliuawa huku raia wengi wakilazimika kutoroka.

Muhariri wa BBC anayesimamia maswala ya afrika amesema kuwa kundi la Alshabaab litahisi athari za kutekwa kwa mji wa Koryoley kwa kuwa ulikuwa makaazi ya wapiganaji wengi wa kigeni na njia ya kuelekea katika makao makuu ya wapiganaji hao ya Barawe.