Wamuua binti kwa 'kosa la ndoa' India

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mauji kama haya sio jambo la kawaida kutokea maeneo ya Kusini mwa India

Polisi nchini India wamesema kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 26 mtaalamu wa Komputa, amepatikana akiwa amenyongwa nyumbani kwao.

Wazazi wa mwanamke huyo ambao wanazuiliwa na polisi wamekiri kumuuza binti yao kwa sababu aliolewa kinyume na matakwa yao.

Mwanamke huyo aliolewa na mfanyakazi ,mwenzake kutoka jamii tofauti siku chache zilizopita.

Maafisa wanasema kuwa mauaji kama haya sio kawaida kutokea maeneo ya Kusini mwa India.