Reeva Steenkamp alimuogopa Pistorius

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Oscar na merehemu Reeva

Aliyekuwa mpenzi wa Oscar Pistorus, marehemu Reeva Steenkamp, alimtumia ujumbe wa simu kumwambia kuwa wakati mwingine alikuwa anamuogopa sana.

Haya yamejitokeza katika kesi inayoendelea dhidi ya Oscar Pistorius nchini Afrika Kusini.

Ujumbe huo aliutuma Reeva baada ya wawili hao kugombana alipomtuhumu kwa kutongozana na mwanamume mwingine...wiki chache kabla ya kumuua.

Afisa mmoja wa polisi ndiye amekuwa akitoa ushahidi dhidi ya Pistorius hii leo.

Pistorius amekanusha madai ya kumuua kwa maksudi mpenzi wake akisema kuwa alifyatua risasi akidhani alikuwa anampiga mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.

Reeva alikuwa amemlalamikia Pistorius kwa kumwambia kuwa anahitaji ulinzi zaidi kutoka kwake kwani hawezi kushambuliwa na watu wa nje kwa sababu ya kuwa na uhusiano nae wakati yeye mwenyewe pia anamshambulia''

Kesi hiyo, imeingia sasa wiki yake ya nne huku upande wa mashitaka ukitarajia kumaliza kuwailisha kesi yake siku ya Ijumaa.

Afisaa huyo wa polisi alisema kuwa alipata ujumbe wenye kurasa 35,000 katika simu ya Steenkamp.

Bwana Pistorius aliambia mahakama kuwa alisahahu nambari ya siri ya simu yake punde mauaji yalipofanyika hali iliyolazimisha polisi kuenda Marekani kuitaka kampuni ya Apple kuwawezesha kufungua simu ya Oscar ambayo ni ya Apple