Jamaa wa abiria wa MH370 wakabiliana na polisi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Familia za abiria waliokuwa kwenye ndege ya MH370

Familia za abiria wa ndege iliyotoweka ya Malaysia majuma mawili yaliyopita, wamekabiliana na polisi nje ya ubalozi wa Malaysia mjini Beijing.

Wakiwa wamejawa na ghadhabu, wamelitaka shirika la ndege ya taifa hilo mjini Kuala Lumpur kueleza kilIchofanyika.

Jamaa hao walibeba mabango yenye maandishi "Save MH370" jamaa hao wenye hasira walikabiliana na polisi na kuwalemea hadi kuingia katika ofisi ya ubalozi huo.

Walifoka wakisema ..''Tunataka ukweli." hii ni ishara ya hasira na mafadhaiko wanayopitIa jamaa hao wa watu waliopotea.

Kero la jamaa hao limekuja baada ya waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak kusema udadisi wa data ya Satelite ulionyesha kuwa safari ya ndege hiyo iliishia baharini Kusini mwa Australia.

Serikali ya China imeomba kuona data hiyo ambayo Malaysia imeamini kiasi cha kutoa msimamo wake.

Haki miliki ya picha
Image caption Msako wa ndege hiyo umesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini

Shughulii ya kuitafuta ndege hiyo MH370 imesitishwa kutokana na mawimbi makali baharini.

Mataifa mbali mbali yalijitolea kusaidia Malaysia kuitafuta nmdege hiyo, juhudi ambazo zililengwa zaidi katika bahari ya Kusini Magharibi mwa mji wa Australia Perth

Ndege hiyo MH370 ilipotea tarehe nane mwezi Machi, ilipokuwa njiani kuelekea Beijing kutoka Kuala Lumpur.

Ilikuwa imebeba abiria 239 ikiwemo raia 153 wa China.

Maandamano ya umma ni haramu nchini China,lakini hadi kufikia watu hawa wakapanga maandamano kama hayo ni ishara kuwa hawana kilichobakia kuwapa matumaini kabisa.