AU:Anti Balaka ni kundi la maadui

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kundi la Anti-Balaka

Mkuu wa vikosi vya Afrika vya kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ,amesema kuwa vijana wa kulinda amani wa kikristo wanaojulikana kama anti-balaka,watatambulika kama maadui kutoka sasa.

Tangazo hilo la Jean -marie Michel Mokoko linajiri baada ya kadhaa za mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya watu 20.

Kundi la Anti-balaka limefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya waislamu baada ya waasi wa kiislamu wa kundi la seleka kuchukua mamlaka mwaka mmoja uliopita.

Jenerali Mokoko pia amelilaumu kundi hilo la anti-balaka kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya kulinda amani vya Afrika vinavyoshirikiana na wenzao wa Ufaransa ili kuzipokonya silaha pande husika.

Mkuu wa kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu Peter Maurer ameanza ziara yake ya siku tatu nchini humo. Kamati hiyo inasema kuwa taifa hilo linakumbwa na janga la kibinaadamu.