Rufaa ya mfungwa miaka 46 baadaye

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kesi ya lwao Hakamada kusikizwa upya

Mwanamme mmoja raia wa Japan ambaye amekuwa kuzuizini kwa kipindi cha miaka arobaini na sita amepewa ruhusa ya kusikilizwa tena kesi yake.

lwao Hakamada mwanandondi wa zamani alihukumiwa kifo na anakisiwa kuwa amekuwa kizuizini kwa kipindi kirefu zaidi.

Hakamada alikutwa na makosa ya kumuua msimamizi wake , mkewe na wanawe wawili kwenye kiwanda kimoja cha nafaka.

Mahakama kwenye mji wa Shizuoka ilitupilia mbali hukumu ya kifo aliyopewa kutokana na tashwishi zilizoibuka wakati wa kesi yake..

Bwana Hamaka awali alikuwa amekataa makosa hayo lakini akayakubali badaaye kutokana na kile alichodai kuwa dhuluma kutoka kwa polisi waliokuwa wakimhoji.