Wanajeshi wa Marekani wafutwa kazi

Image caption Wanajeshi 9 wa kinyuklia wafutwa kazi kwa udanganyifu

Jeshi la angani la Marekani limewafuta kazi maafisa wake tisa katika kambi moja ya silaha za kinyuklia baada ya kudanya katika mtihani.

Afisa mwengine katika kambi hiyo ya Malmstrom mjini Montana amejiuzulu.

Wachunguzi wanasema kuwa maafisa hao wa jeshi walihisi kulazimishwa kupasi asilimia 100% katika kila mtihani.

Uchunguzi huo umebaini kuwa maafisa hao hawakushiriki katika udanganyifu lakini walishindwa kutoa usimamizi wa kutosha

Udanganyifu huo ulibainika kufuatia uchunguzi wa utumizi wa mihadarati katika kambi hiyo.