Uvutaji sigara unawaathiri watoto

Haki miliki ya picha PA
Image caption Uvutaji sigara unaathiri afya ya kina mama wajawazito

Utafiti mpya kutoka ulaya na marekani kazkazini unasema kuwa,kupigwa marufuku kwa uvutaji wa sigara hadharani kumesababisha kushuka kwa viwango vya wanawake kujifungua mapema kabla ya mda wao kwa asilimia 10.

Idadi ya watoto waliolazwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa pumu pia imepungua kwa asilimia 10% katika maeneo ambayo uvutaji sigara hadharani umepigwa marufuku kulingana na wanasayansi kutoka chuo cha Edinburgh nchini Scotland.

Mmoja ya waanzilishi wa utafiti huo Prof Aziz Sheikh ambaye ripoti ya utafiti wake imechapishwa katika jarida la matibabu duniani Lancet,anasema kuwa mataifa yasio na marufuku hiyo yanapaswa kutilia maanani matokeo hayo kwaajili ya kizazi chao cha baadaye.

Kwa sasa ,sheria dhidi ya uvutaji sigara zinaathiri asilimia 16 ya idadi ya watu dunaini.