Mahabusu 21 wauawa Nigeria

Haki miliki ya picha
Image caption Polisi Nigeria wamesema wafungwa 21 waliuawa

Wafungwa 21 waliuawa walipojaribu kutoroka kutoka kwenye makao makuu ya Kitengo cha Jinai cha jeshi la polisi la Nigeria lililoko Abuja.

Hadi kufikia sasa haijabainika iwapo waliokufa wote ni wafungwa au la .

Msemaji wa kitengo hicho cha jinai Marilyn Ogar , amesema maafisa wawili wa kitengo hicho walijeruhiwa vibaya ,mahabusu walipowavamia kwa pingu zao .

Watu walioshuhudia wanasema milio ya risasi ilisikika karibu na kasri la rais punde baada ya jeshi la taifa kuingilia kati kuzima jaribio hilo la kutoroka kwa mahabusu.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa gereza hilo linakisiwa kuwa limehifadhi wapiganaji wa kundi lililopigwa marufuku, la Boko Haram.