Ebola yafanya Senegal kufunga mpaka

Daktari wa Guinea kwenye maabara Haki miliki ya picha

Senegal imefunga mpaka wake na Guinea katika juhudi za kuzuwia virusi vya Ebola ambavyo vimeuwa watu kama 70 nchini Guinea.

Wagonjwa wengi waliopata Ebola wako kusini magharibi mwa Guinea, lakini watu kama wanane katika mji mkuu, Conakry, wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo.

Wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Ebola piya wanachunguzwa katika nchi mbili jirani na Guinea - Liberia na Sierra Leone.