Biashara ya Taiwan na Uchina yapingwa

Haki miliki ya picha Reuters

Makumi ya maelfu ya raia wa Taiwan wamefanya maandamano katika mji mkuu wa Taipei ili kupinga makubaliano ya kibiashara na Uchina.

Wengi ya waandamanaji hao walivalia mashati meusi pamoja na vitambaa vya manjano kichwani mbali na kubeba mabango yaliosema 'linda demokrasia vunja mkataba wa kibiashara'.

Wanasema makubaliano hayo yataifanya Taiwan kuitegemea Uchina kwa kiasi kikubwa katika maswala ya kiuchumi.

Rais wa Taiwan Ma Ying Jeou,amesisitiza kuwa mkataba huo ni mzuri kwa uchumi wa Taiwan.

Maandamano ya leo yanaunga mkono wanafunzi ambao wamelithibiti jengo la bunge la Taipei kwa kipindi cha majuma mawili yaliopita wakipinga mpango huo wa biashara.