Jenerali wa jeshi ashitakiwa kwa ufisadi China

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano ya kupinga ufisadi nchini China

Viongozi wa mashitaka nchini China wamemfunguliwa mashitaka ya ufisadi na utumizi mbaya wa mamlaka afisaa mmoja mkuu wa zamani wa jeshi nchini humo.

Kesi hii inafanyika wakati Rais wa China akizindua kampeni kali ya kupambana na ufisadi ambayo tayari imewalenga maafisa wakuu wa serikali na maafisa wa chama kikuu cha kikomunisti,

Kampeini hiyo sasa pia inaonekana kuwalenga maafisa wakuu wa jeshi.

Hata hivyo kuna ripoti kuwa maafisa kadhaa wakuu wana wasiwasi kuhusu ikiwa kampeni hiyo huenda ikavuka mipaka.

Luteni General Gu Junshan, alikuwa mmoja wa maafisa wakuu wa jeshi. Lakini inadaiwa kuwa aliishi maisha ya kifahari na kumiliki mali ya thamani ya mamilioni ya dola.

Vyote hivyo vilitokana na mlungula aliopokea kwa kuuza ardhi ya jeshi na kutoa kandarasi za jeshi wakati alipokuwa naibu mkuu wa utaratibu jeshini.

Rais Xi Jinping, amekuwa akitumia kampeni hiyo kuonyesha nguvu zake katika chama tawala lakini sasa anaonekana kuligusa jeshi katika harakati zake dhidi ya ufisadi.

Lengo la kempeini yake ni kuimarisha imani ya watu katika chama tawala.

Duru zinasema kuwa Rais wa zamani Jiang Zemin, amemwandikia barua Rais na kumsihi kutovuka mipaka katika kampeini yake dhidi ya ufisadi.