Urusi yawanasa raia 25 wa Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Urusi imewakamata raiya 25 kutoka Ukraine

Kitengo cha kimataifa cha upelelezi Nchini Urusi FSB, kinasema kuwa kimewazuilia raia 25 wa Ukraine, kikiwalaumu kwa kupanga mashambulio ya kigaidi mwezi uliopita wakati jimbo la

Crimea lililoko Ukraine lilipokuwa likiandaa kura ya maoni.

Idara hiyo inasema watu hao wanaozuiliwa walikuwa wanachama wa vuguvugu la ultra-nationalist na walikuwa wakijiandaa kusababisha mashambulio hayo katikati na Kusini mwa Urusi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kikosi cha polisi cha Berkut chalaumiwa kwa vifo wakati wa maandamano

Awali, waziri wa usalama wa taifa wa Ukraine, Arsen Avakov amesema kuwa tume rasmi ya uchunguzi inaonyesha kuwa kitengo maalum cha polisi kiitwacho Berkut kilichobuniwa kukabiliana na vurumai kiliwauwa waandamanaji kadhaa katika uwanja wa maandamano mjini Kiev, mwezi Februari.

Amesema kikosi hicho maalum cha polisi kimevunjiliwa mbali.

Kaimu Waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk ameiambia BBC kuwa rais aliyeng'olewa madarakani Viktor Yanukovych na washirika wake ndio wahusika wakuu katika maafa hayo.

Zaidi ya watu 100 waliuwawa katika vurumai hilo.

Naye kiongozi mkuu wa upelelezi Nchini Ukrainne Valentyn Nalyvaychenko amesema kuwa idara ya upelelezi ya Urusi imetuma tani kadhaa za villipuzi na silaha hadi Ukraine.