Pistorius aendelea kutoa Ushahidi wake

Image caption Pistorious mahakamani kutoa ushahidi

Mwanariadha mlemavu mshindi wa nishani za dhahabu za olimpiki Oscar Pistorius ameanza kutoa ushahidi wake kwa siku ya pili katika kesi ya mauaji inayomkabili kuhusiana na kifo cha mchumba wake wa zamanai Reeva Steenkamp.

Akizungumza kwa sauti ya kutetema,Pistorious amesema hakukusudia kumuua Steenkamp na kuwa alidhania kuwa amevamiwa na wezi nyumbani kwao.

Iwapo atapatikana na hatia mwanariadha huyo anakabiliwa na hukumu ya kifo.

Hapo jana Pistorious aliiomba radhi familia ya Steenkamp akisema kuwa hakuna hata siku moja tangu siku hiyo aliyokufa ambayo hajamfikiria mpenzi wake .

Pistorius amesema kuwa mara nyingi ameamka na kusikia harufu ya damu ya Bi Steenkamp.

Image caption Mamake Reeva akimsikiza Pistorious mahakamani

Waendesha mashtaka wanasema Pistorius alimuua Steenkamp mwezi Februari 2013 baada ya kuzozana.

Pistorius anaulizwa maswali na upande wa mashtaka kubwa ikiwa ni jumbe za simu ya mkononi ambayo ilipatikana katika simu ya Steenkamp na inaonesha kuwa mwanadada huyo alikuwa anaogopa tabia na miondoko ya

Pistorious akipandwa na mori .

Amesema anatumia dawa za kuzuia msongo wa akili na kukosa usingizi.

Mamake Steenkamp June alikuwa miongoni mwa watu waliojaa mahakamani huko Pretoria kusikiza ushahidi wake .

Mahakama hiyo imekwisha sikiza upande wa mashtaka ambao ulitegemeakwa kiasi kikubwa ushuhuda wa majirani maafisa wa polisi waliotangulia katika eneo la tukio , watafiti wa risasi na vilipuzi mbali na jumbe za simu ya mkononi .

Mwanamitindo huyo aliyekuwa amekuwa maarufu kutokana na maonyesho yake kwenye runinga alikuwa amemzomea Pistorius kwa kupandwa na hasira kila anaposhuku kuwa alikuwa anazungumza na wanaume wengine.

Kesi inaendelea huko Pretoria .