UN yawatelekeza wakimbizi Sudan Kusini ?

Image caption Maji taka yamezagaa katika kambi ya Umoja wa mataifa ya wakimbizi Sudan Kusini

Umoja wa mataifa Nchini Sudan Kusini umejitetea vikali kutokana na ukosoaji kwamba inawabagua watu wanaotaabika ndani ya makao yake makuu katika jiji kuu la Sudan Kusini Juba.

Wakimbizi hao wamekita kambi kwenye ofisi za umoja wa mataifa baada ya kukimbia mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kirr Mayardit na aliyekuwa makamu wake Riek Machar.

Mnamo jumatano wiki hii, kundi la madkatari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres lilisema kuwa watu elfu 20 wanaishi katika hali ya mateso makubwa baada ya mvua iliyonyesha majuzi na kusababisha vyoo kufurika na

kuporomoka.

Toby Lanzer, naibu mkuu wa umoja wa mataifa mjini Juba ameiambia BBC kuwa wanatamaushwa pia na hali mbaya ya maisha ya watu hao waliokimbia mapigano.

Lakini amesema kuwa kambi hiyo ya muda haikuwa ihudumie idadi kubwa ya watu.

Aidha amesema kuwa wanafanya kila wawezalo ili kuboresha sehemu hiyo mbali na kujaribu kukodisha shamba lililo maeneo ya nyanda za juu viungani mwa mji mkuu ili kujenga kambi nyingine ya muda ya kuwahudumia watu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Umoja wa mataifa wawatelekeza wakimbizi Sudan Kusini

Shirika moja lisilo la kiserikali la madaktari wayo na mipaka , Medecins Sans Frontieres (MSF) lilitoa picha na habari zilizosimulia hali mbaya wanayostahimili wakimbizi wa ndani kwa ndni nchini Sudan Kusini huku Wafanyikazi wa

shirika la umoja wa mataifa linalosimamia maswala Sudan UNMISS likipuzilia mbali masaibu yao.

MSF ilitoa picha ya Kambi hiyo ambayo inawatu takriban 21,000 wakiishi katika kambi ambayo maji taka yamezagaa kwote .

Shirika hilo lilitoaushahidi kuwa vyoo 150 vya kambi hiyo vimeporoka na uchafu umetapakaa ovyo.

Zaidi ya watu milioni moja wametoroka makwao .

Takriban watu , 803,200 ni wakimbizi wa ndani kwa ndani huku wengine 254,000 wametorokea nje ya nchi.