Wahoji kilio cha Pistorius mahakamani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Oscar Pistorius amekana kumuua mpenzi wake kwa maksudi

Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayoendelea nchini Afrika Kusini dhidi ya Oscar Pistorius, umehoji kilio cha Pistorius ukisema kuwa anatumia machozi yake kama kisababu cha kutaka kuhurumiwa na kuoteza ushahidi.

Oscar aliangua kilio mahakamani Jumatatu na hata kutapika.

"sasa unajaribu kujifanya una masikitiko, lakini hiyo haitakuondoa kutoka katika kesi hii,'' alisema mwendesha mashitaka Gerrie Nel.

Bwana Pistorius anakiri kumuua mpenzi wake marehemu Reeva Steenkamp mwezi Februari, mwaka jana lakini anasema kuwa alifyatua bunduki yake baada ya kushuku kuwa mtu alikuwa amevamia nyumba yake.

Kwa upande wake bwana Nel alisema kuwa mwanariadha huyo,mwenye umri wa miaka 27, alimuua mpenzi kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.

Image caption Nyumba ya Pistorius

Huku akianza kumhoji Oscar, alimtuhumu Pistorius kuwa alitumia udanganyifu katika ushahidi wake kama njia ya kujiondoa katika kesi hiyo.

''Ushahidi wako umajaa uongo,'' alisema bwana Nel.

Huku akiangua kilio, Oscar Pistorius alisema, ''sikumlenga Reeva wakati nilipofyatua risasi.''

Kabla ya kesi kuahirishwa, Nel alimwambia Pisorius, "unaanza kulia kwa sababu unahisi kuwa ushahidi wako umejaa chembechembe za uongo na kwa hivyo haukusaidii kwa njia yoyote.

Hii sio mara ya kwanza kwa Oscar Pistorius kuangua kilio mahakamani , amelia sana kufuatia kifo cha mpenzi wake, lakini wendesha mashitaka wanahisi kuwa Pistorius anatumia machozi yake kama kama kisibabu cha kutaka kuhurumiwa .